![](../sites/default/files/core%20values%20of%20decentralization_1.jpg)
MUHTASARI
Haja ya kushughulikia maswala ya upatikanaji wa nishati kusini mwa dunia - umeme na upishi safi kwa pamoja - ni ya haraka na inazidi kutambuliwa kuwa muhimu kufikia malengo mapana ya maendeleo. Walakini, kinachoeleweka sana kwa umbali ni kwamba ugatuzi wa madaraka (uhamishaji wa mamlaka kutoka kwa serikali kuu hadi zile za mashinani) una umuhimu wazi na dhahiri kwa sekta ya nishati na inatoa fursa muhimu za kuharakisha upatikanaji wa usawa zaidi wa huduma za kisasa za nishati. Kwa kuzingatia matokeo ya mradi wa utafiti wa miaka minne1 katika ugatuzi wa utawala wa nishati nchini Kenya, muhtasari huu wa sera unaonyesha umuhimu wa ugatuzi wa madaraka kwa nishati, majukumu yanayoweza kufanywa na taasisi za mashinani, na changamoto zinazoweza kutokea kuhusiana na utekelezaji na matokeo ya sera. Tofauti dhahiri za kijiografia katika ubora wa utawala katika kaunti nne zilizo fanyiwa utafiti pia zinafunuliwa.
Utangulizi
Ugatuzi- uhamishaji wa mamlaka, nguvu, rasilimali, na majukumu kutoka kwa wahusika wa ngazi ya kati(kitaifa) hadi ya chini (wa mashinani zaidi) - umekuwa mchakato wa kisiasa katika nchi nyingi ulimwenguni2. Watetezi wa ugatuzi wanasema ugatuzi huleta utawala wenye habari zaidi, msikivu, na uwajibikaji, ambayo inawezesha demokrasia zaidi na kuboresha utoaji wa huduma3. Wakosoaji wamebaini kwamba faida za ugatuzi zinazodhaniwa, mara nyingi huzuiliwa na uwezo wa serikali za mitaa, na kusita kwa serikali kuu kuwapa nguvu muhimu na rasilimali4.
Kusini mwa ulimwengu5, ugatuzi wa madaraka umetetewa na mashirika ya maendeleo tangu miaka ya 1970 kama njia ya kuboresha utawala na utoaji wa huduma kwa kuzuia rushwa inayodhaniwa, na siasa za serikali kuu6. Walakini, licha ya ugatuzi kutekelezwa mara kwa mara katika mipango ya maendeleo katika sekta muhimu kama vile maji, afya na kilimo, umakini mdogo umepewa jinsi utawala wa serikali unaweza kushughulikia masuala ya upatikanaji wa nishati. Hasa, watu milioni 770 ambao hawana huduma ya umeme, na watu bilioni 2.6 bila vifaa safi vya kupikia7. Lililo tajwa wisho ni la kupewa kipao mbele zaidi kwa sababu ya athari mbaya ya mazingira na afya kutokana na upishi kupitia nishati inayochafua kama kuni na makaa, na matokeo ya uchafuzi wa hewa kwenye maboma unasabisha vifo vya mapema vya watu milioni 4 kila mwaka8.
VIDOKEZO MUHIMU
• Ugatuzi una umuhimu wazi na dhahiri kwa maswala ya ufikiaji wa nishati Kusini mwa dunia.
• Kukosekana kwa usawa wa nguvu kumesababisha maswala ya upatikanaji wa nishati kushughulikiwa kidogo nchini Kenya kwa sababu ya mkazo mkubwa juu ya umeme ya gridi ya taifa, huku wakipuuzilia mbali mahitaji ya haraka ya umeme wa kiwango kidogo wa inje ya gridi na uanzishaji wa nishati safi ya kupikia.
• Tofauti za kijiografia za ubora wa utawala ziko wazi katika ngazi ndogo za kitaifa.
UJUMBE WA SERA
Jukumu muhimu la utawala wa nishati uliogatuliwa ni kukuza na kudumisha mitandao ya watendakazi wa mashinani kutetea na kuwezesha suluhisho inayofaa zaidi ya upatikanaji wa nishati (haswa safi ya kupikia na wa kiwango kidogo inje ya gridi), ilihali wakifanya ukaguzi mzuri wa serekali kuu na kuiweka kwenye mizani. Ili kuwezesha jukumu hili, yafuatayo yanapendekezwa:
• Uainishaji wazi wa sheria kati ya majukumu ya kitaifa na yale ya ngazi ndogo za kitaifa
• Kanuni zilizoboreshwa ili kuwezesha ugatuzi wa umeme wa inje ya gridi.
• Usawa zaidi wa kijiografia wa kujenga uwezo.
• Ongezeko la uhusishaji wa jamii
• Jukumu la mwezeshaji (badala ya mtekelezaji) lililopitishwa na serikali ndogo ya kitaifa, kuratibu mitandao ya wafanyi kazi wa mashinani ili kuendeleza mipango inayofaa ya nishati.
Umuhimu wa ugatuzi
Ugatuzi wa madaraka ni muhimu sana kwa nishati kwani mchakato huo unaweza kusaidia kushughulikia kasoro za utawala wa kati, ambazo zimeonekana kama sababu kuu inayokwamisha upatikanaji wa nishati kwa usawa - haswa katika Kusini mwa Jangwa la Sahara (KJS). Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan alisisitiza kuwa:
Kwa muda mrefu sana, viongozi wa Afrika wamekuwa wakiridhika kusimamia mifumo ya nishati iliyolimbikizwa sana sehemu moja na iliyoundwa kufaidi matajiri na kuwapita maskini… Utawala wa huduma za umeme ndio kiini cha shida ya nishati barani Afrika9.
Serikali kuu zimekuwa "zinaridhika kusimamia mifumo ya kati ya nishati" kwa sababu huduma za gridi ya taifa (haswa usafirishaji na usambazaji (U&U)) huwa na nguvu usiyo na msimamo rasmi ya ukiritimba kusini mwa dunia. Kwa kuzingatia tabia ya kutafuta kodi ndani ya ukiritimba kama huo na faida kubwa ya sekta ya nishati, serikali kuu zimefanya kazi ya kulinda maslahi yake ya gridi10. Walakini, miundombinu dhaifu ya U&U imeacha umeme wa gridi kutoaminika na ni ghali na viwango vya ufikiaji Kusini mwa Jangwa la Afrika ni miongoni mwa viwango vya chini kabisa ulimwenguni11. Suluhisho za nje ya gridi ya taifa limepuuzwa licha ya kuwa chaguo la gharama ya chini zaidi kwa 55% Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata ufikiaji wa umeme ifikapo 203012. Upishi safi nao umepokea uwekezaji mdogo zaidi chini ya sera ya gridi iliyolimbikizwa sehemu moja13.
Uwezo wa utawala uliogatuliwa.
Utafiti katika utawala wa nishati uliogatuliwa kusini mwa dunia umekuwa na vikwazo lakini tafiti chache zilizopo zinasisitiza faida za utawala kama huo: haswa, udemokrasia mkubwa wa nishati, na ufanisi bora wa nishati, usalama, uthabiti, na uwezo wa kumudu14. Ugatuzi wa madaraka unajulikana kwamba una "umuhimu maalum" kwa nishati ya nje ya gridi kwani zote zinahusu kubadilisha uhusiano kati ya viwango tofauti vya shughuli na msisitizo mkubwa kwa viwango vidogo15. Wasomi wanashauri kwamba tawala zote mbili zinahitaji kuzingatiwa kwa pamoja ili kuongeza fursa zaidi, lakini wanaonya kwamba kutawala kwa maslahi ya gridi kuu ni kikwazo kikubwa cha uchumi wa kisiasa16.
Uchunguzi pia unaonyesha kwamba ugatuzi una umuhimu tofauti kwa nishati kwa sababu ya ugumu utokanao na miundombinu tata ya nishati kwa utawala bora, haswa suluhisho ya miundombinu inayopima viwango vingi na mamlaka tofautu tofauti (k.v kitaifa na mitaa). Kuingiliana huku kunaweza kusababisha uhasama kati ya mabaraza yaliyogatuliwa madaraka na taasisi zilizopo madarakani, mashirika ya udhibiti, na watendaji soko17. Ili kushughulikia maswala haya, wasomi wakuu wa nishati wanasisitiza kwamba utawala unahitaji kujumuisha njia zote za ugatuzi na zile zilizolimbikizwa sehemu moja kwani "hii inaruhusu utafutaji wa muktadha, majaribio na uvumbuzi, ambayo inaweza kusababisha suluhisho za miundombinu endelevu na ujifunzaji katika mizani tofauti tofauti"18. Walakini, katika njia hizi, majukumu tarajiwa ya taasisi zilizogatuliwa bado hayaeleweki vizuri.
Hivyo basi, muhtasari huu wa sera unachunguza mchakato wa ugatuzi wa nishati ya Kenya na mienendo muhimu ya nguvu (uchambuzi wa kwanza wa aina hii katika Kusini mwa dunia) kutathmini majukumu muhimu ambayo taasisi zilizogatuliwa zinaweza kupewa, changamoto tarajiwa za utekelezaji na mwitikio tarajiwa wa sera hii. Tofauti kubwa katika ubora wa utawala katika utafiti wa Kaunti manne - Migori, Nakuru, Nairobi, na Turkana (Kielelezo 1) - pia imeangazia.
Kielelezo 1. Kaunti za utafiti
Ugatuzi wa Kenya
Iliundwa mnamo mwaka wa 2013 (kufuatia kupitishwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010), ugawanyaji wa madaraka nchini Kenya umetajwa kama "kati ya michakato ya ugatuzi ya haraka na kabambe duniani”19. Kaunti 47 mpya ziliundwa, kila moja ikiwa na: serikali ziliyochaguliwa iliyo na mamlaka ya kisiasa, kifedha na utawala juu ya utoaji wa huduma muhimu; dhamana ya angalau 15% ya mapato ya kitaifa; na ulinzi wa kikatiba kwa mtendaji wa kaunti. Mfumo wa Kenya "mfano wa-ushirikisho"20 umetajwa kama "mageuzi ya kweli" badala ya (kama inavyoonekana katika michakato mingine ya ugawanyaji wa mamlaka KJS) hatua ya kijuujuu, ambayo inaunganisha mamlaka kuu kwa kejeli tu21.
Maendeleo ya sekta ya nishati baada ya mwaka wa 2013
Licha ya muktadha wa sheria kuonekana kuwa mzuri kwa utawala uliogatuliwa, sekta ya nishati baada ya kugawa madaraka imebaki kutawaliwa na serikali ya kitaifa ambayo inaonekana kusita kuachia madaraka madhubuti. Masilahi ya serikali ya kitaifa katika upanuzi wa gridi ya taifa na mipango ya 'kisiwa cha gridi'22 imekuwa ikipewa kipaumbele kupita kiasi. Japo imsababisha ikuongezeka kwa upatikanaji wa umeme, huo umekuwa kiwango cha chini na bila usawa. Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa ufikiaji uliongezeka kutoka 32% ya kaya mnamo 2013 hadi 75% mnamo 201823. Takwimu hizi zinaonyesha upatikanaji tu lakini matumizi halisi ni ya chini sana kwani kaya nyingi haziwezi kumudu kulipia umeme uliopo24. Kudumisha maunganisho ya kufanya hasara na uzalishaji umeme ya ziada (kwa sasa 500MW) hugharimu gharama ambazo hupitishwa kwa watumiaji, ikizuia zaidi uwezo wa kumudu na kuchukua umeme25.
Kuzingatia gridi ya taifa pia kumefanya umeme mdogo wa gridi ya inje na upishi safi kupuuzwa. Zote zinahitajika haraka. Angalau 10.2% ya kaya zote nchini, zaidi sana kaunti za Ukame na Nusu-Kame (KUNK) zilizotengwa kihistoria, ziko nje ya uwezo wa gridi inayofaa na zinahitaji suluhisho za nje ya gridi26. Kwa kuongezea, 80% ya waKenya bado wanapikia kuni na makaa, na kusababisha vifo vya watu 21,650 kila mwaka27. Njia za sasa zinazofuatwa na serikali zitaona Kenya ikikosa malengo yake ya 2028 SE4All ya ufikiaji wa upishi safi28.
Athari za uhusiano wa nguvu tawala.
Utawala unaoendelea wa ulimbikizaji mamlaka sehemu moja umeungwa mkono na ukosefu mkubwa wa usawa wa nguvu: Matumizi ya serikali ya kitaifa ya udhibiti wa sheria, kanuni na rasilimali zimetumika kuweka kipaumbele katika sera ya gridi na kuzuia maendeleo ya utawala wa nishati.
Ubaya zaidi kwa utawala wa chini nikwamba serikali ya kitaifa kwa muda mrefu imeshindwa kuunda mfumo wazi wa sheria ya nishati. Katika uzinduzi wa Katiba ya 2010, kulikuwa na uelewa wa kimyakimya wa hitaji la kufafanua majukumu ya nishati kwani Katiba ilitoa muhtasari mpana tu, ikitoa mamlaka muhimu ya upangaji wa nishati kwa kaunti lakini haitoi maelezo yoyote ya mipango hii inavyopaswa kujumuisha (Jedwali 1). Majukumu ya kaunti na kitaifa ya usambazaji na udhibiti pia yalikuwa na mwingiliano29, na kusababisha kutokuwa na uhakika na majukumu kutafsiriwa vibaya30.
Jedwali 1. Majukumu ya Nishati chini ya katiba
Walakini, muswada mpya wa nishati haukutolewa hadi 201531. Ulipopitishwa na bunge, muswada huo ulipigwa kura ya turufu na Rais mnamo 2016 kwa sababu mtendaji mkuu alitaka kupunguza sehemu ya mapato ya petroli yaliyotengwa kwa kaunti na jamii za wenyeji - suala lililokuwa mashuhuri baada ya kupatikana kwa mafuta katika Kaunti ya Turkana mnamo 2012. Kura hii ya turufu ya kujitumikia ilizingatiwa sana kama kizuizi kikuu cha ugatuzi wa utawala wa nishati kwa kuwa iliacha Sheria ya Nishati 2006 kama sheria ya utendaji, sheria ambayo ilitangulia ugatuzi na haikutaja majukumu ya kaunti, ikasababisha utupu wa kisheria ambao ulikosesha kaunti uharaka na nguvu ya kufanya kazi32.
Ufafanuzi wa kina wa majukumu ya kitaifa na kaunti ulianza 2019 na kupitishwa kwa Sheria ya Nishati 2019. Sekta hiyo iligatuliwa kwa kiasi tu lakini kutokuwa na uhakika kuliendelea kwani majukumu mengi hayakukuwa na mipaka wazi ya wapi majukumu ya kitaifa na kaunti yalianzia na kuishia, ikizuia uratibu. Majukumu muhimu ya umeme yalibaki katika kiwango cha kitaifa, pamoja na sera, kanuni, uzalishaji, na usambazaji. Mashirika ya umma (kwa mfano KPLC, EPRA na KenGen)33 yanayotawala maeneo haya pia yalibaki kutawaliwa na serikali ya kitaifa. Mashirika haya yalifanya marekebisho machache tu ya kiutawala (kama vile kufungua ofisi za kaunti) kukidhi ugatuzi.
Kwa kweli, kulikuwa na kifungu kidogo cha uamuzi wa uhuru, ulioboreshwa kwa kaunti wakati usimamizi wote wa sekta ya umeme uliendelea kushikiliwa na serikali ya kitaifa34. Ingawa hii inaeleweka na umeme wa gridi kusaidia uratibu wa kitaifa, hitaji la ruhusa za serikali ya kitaifa kwa mipango midogo ya nje ya gridi haina maana, haswa wakati ambapo mitandao ya wahusika wa ugatuzi imekuwa madereva wa msingi kwa mipango ya nje ya gridi35 na ina uwezo mkubwa wa kuwezesha mipango ya upishi safi36 inayohitajika upesi. Mifumo ya nje ya gridi inaweza kufanya kazi kwa kujitegemea au sambamba na gridi ya taifa. Usimamizi huu mkali wa udhibiti umezuia na kuua motisha ya hatua za kaunti37.
Ukosefu wa majukumu wazi ya nishati ya kaunti na urekebishaji mdogo wa sekta ya umeme unaonekana kumaanisha kuwa ugatuzi wa kiutawala (au 'upunguzaji wa sheria') ndio serikali ya kitaifa ingependelea, badala ya ugawanyaji wa uhuru, kisiasa na kifedha ambao unaweza kusababisha rasilimali na mapato kutolewa kutoka katikati. Rasilimali zimejikita katika masilahi ya serikali ya kitaifa badala ya mipango midogo ya nje ya gridi na upishi safi ambapo serikali ya kitaifa ingekuwa na udhibiti mdogo38. Kwa kuwa nishati ni mojawapo ya wizara tatu zenye faida kubwa39 na inadaiwa kushikiliwa na wasomi40, upendeleo wa serikali kuu wa upunguzaji wa sheria unaonekana kuonyesha jinsi nishati, zaidi ya sekta zingine, inavyoonekana kuwa muhimu sana kisiasa na kifedha kugatuliwa kikamilifu.
Uwezo
Maswala ya uwezo yamepunguza usimamizi wa nishati uliogatuliwa. Kutokuwa na uhakika juu ya majukumu ya kaunti na usimamizi wa kupindukia wa udhibiti kutoka serekali kuu, kumesababisha kaunti nyingi kutokuwa tayari kutoa rasilimali zao chache kwa sekta hiyo, na karibu nusu ya kauti zote hazikuanzisha idara za nishati41. Tawala nyingi hazina wafanyikazi waliohitimu kutekeleza majukumu muhimu, kama vile kufanya ukaguzi wa nishati, kusimamia portfolio za nishati, na kutathmini sifa za teknolojia tofautu tofautu za nishati ilikufanya maamuzi ya ununuzi42.
Kaunti pia hazijathamini majukumu ya nishati ambayo zingeweza kutekeleza licha ya serikali ya kitaifa kudhibiti juu ya sekta hiyo. Mipango ya Nishati ya Kaunti ya Mda wa Kwanza (CEPs) na Mipango ya Maendeleo Jumuishi (CIDPs) ilipuuza majukumu yanayowezekana katika uundaji wa mahitaji ya gridi pamoja na kuwezesha mipango ya gridi ndogo ndogo na upishi safi inayohitajika kwa haraka- ambayo ina gharama za chini, udhibiti mdogo wa usimamizi, na ambapo serikali ya kitaifa ina udhibiti mdogo wa ukiritimba. Mashuhuri zaidi imekuwa mipango ya taa za barabarani, ambazo zina athari ndogo za maendeleo lakini zinaonekana sana na kwa hivyo zina hadhi ya kisiasa. Taa za barabarani pia ni moja wapo ya kazi maalum za kaunti zilizoorodheshwa wazi (Jedwali 1) na huenda pia zilipewa kipaumbele kwa sababu ya urahisi wa utekelezaji wake43.
Walakini, serikali ya kitaifa inawajibika haswa kwa maswala haya ya uwezo kwani kikatiba inahitajika kujenga uwezo wa kaunti, lakini imetoa msaada usio tosha. Mfumo wa upangaji wa kitaifa wa kuongoza na kusanifisha CEPs ulikamilishwa tu mnamo 2018 na bado inapaswa kutolewa kwa ufanisi44. Msaada kwa kaunti pia umepunguzwa kutokana kwamba wafadhili wakubwa wa kimataifa (kwa mfano Benki ya Dunia, UNDP) ambao kimsingi wametumia serikali ya kitaifa kama njia ya kusambaza fedha na msaada, na kupelekea rasilimali zikilenga vipaumbele vya gridi ya serikali ya kitaifa45. Wahusika wengine wachache wa kimataifa, kitaifa, na wenyeji wamehusika katika kujenga uwezo wa kaunti, lakini hatua zimekuwa hazina usawa kijiografia: kaunti zingine zimepokea msaada zaidi kuliko zingine kwa sababu ya uchumi wa kisiasa kama vile uhusiano uliokuwepo hapo awali au masilahi yaliyokuwa kwenye mipangilio haswa teknolojia za nishati au fursa za biashara46. Kaunti ambazo hazina huduma hizi zina upeo mdogo wa kushawishi msaada zaidi na zinajihatarisha kuachwa nyuma.
Ushirikisho wa kiwango cha jamii na haki za ardhi
Ukaguzi wa utawala wa serikali ya kitaifa umekuwa kidogo, lakini umetokea zaidi ambapo mwamko wa jamii na nia ya kuandamana juu ya haki za ardhi zilizoathiriwa na miradi ya nishati imesababisha nguvu na shinikizo toka chini hadi juu. Kesi kama hizo zimesababisha visa vichache ambapo wadau kutoka viwango vyote wamelazimishwa kushirikiana47. Mashuhuri zaidi imekuwa harakati iliyofanikiwa kuongozwa na jamii dhidi ya serikali ya kitaifa iliyopanga kiwanda cha makaa ya mawe kuzalisha 1050MW ya nishati katika Kaunti ya Lamu: mradi ambao sio wa busara ukipewa usambazaji mkubwa wa gridi ya ziada na hitaji la kutegemea makaa ya mawe yenye gharama kubwa wakati rasilimali nyingi za nishati mbadala bado hazijatumika48.
Licha ya mafanikio haya, jamii zimekuwa zikiona thamani kuu ya ugatuzi kama utoaji wa huduma badala ya siasa shirikishi, ikiashiria kwamba uhusiano kati ya jinsi siasa sirikishi huleta utoaji huduma haujafanywa vyema49. Ukosefu wa uhamasishaji wa jamii unawajibika sana50, ingawa sio kweli kwa serikali ya kaunti kuwa na ushiriki wa moja kwa moja wenye maana na kila jamii katika mamlaka yake, na badala yake inahitaji waamuzi wa wajamii (kama vile NGOs / Asasi za Kiraia (CSOs) kuhakikisha mahitaji nishati ya jamii. Hii inamaanisha kaunti zinachukua jukumu la mwezeshaji badala ya mtekelezaji katika mipango ya nishati, na tawala za kaunti zimeweza kukusanya data kutoka kwa waamuzi hawa wa maeneo juu ya asili, kiwango na suluhisho za uwezekano wa maswala ya nishati ya eneo fulani; habari ambayo baadaye wanaweza kuitumia kuelekeza watendaji wanaoona wanauwezo wa kushughulikia maswala haya kwa njia inayofaa kwa muktadha wa mahali hapo.
Tofauti za kijiografia
Ubora wa utawala wa nishati uliogatuliwa umetofautiana sana kati ya kaunti. Hali hii imeungwa mkono na mambo muhimu ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa (Jedwali 2). Uwezo wa idara za nishati za kaunti ndio uamuzi mkuu, ukitofautiana kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya kaunti zilizopea nishati kipaumbele, na kwa hivyo zikatenga rasilimali kwa nishati – yenyewe ikitegemea pakubwa jinsi nishati ilivyokuwa ya muhimu kwenye uchaguzi katika kila kaunti. Kipaumbele kilichopewa utawala wa nishati uliogawanywa pia kiliathiriwa na sababu zingine: kaunti zilizotengwa kihistoria zilionekana kuthamini ugawanyaji wa madaraka zaidi, wakati baadhi ya kaunti zilizo na viwango vya juu vya upatikanaji wa nishati zikitanguliza nishati kwa kiwango kidogo.
Utawala bora zaidi wa nishati uliogatuliwa pia umeibuka katika kaunti ambazo zimepata msaada wa kujenga uwezo na ambapo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na yale ya kiwango cha jamii ni maarufu zaidi katika kutengeneza suluhisho mwafaka wa nishati na kuweza kutumia shinikizo la chini hadi juu kwa utawala wa kati. Jitihada hizi zinaweza kuwa na ufanisi zaidi pale zinaporatibiwa vizuri - jukumu ambalo linaweza kutekelezwa kirahisi na serikali za kaunti.
Jedwali 2. Sababu zinazoathiri ubora wa utawala wa nishati uliogatuliwa.
Jedwali 2 linaangazia jinsi mambo haya yamekuwa dhahiri zaidi huko Turkana kuliko kaunti zingine tatu za utafiti. Turkana imei[a nishati kipaumbele, ikweka wafanyikazi wenye ujuzi katika nafasi muhimu, ambayo imesaidia kaunti katika kupea changamoto serikali ya kitaifa, haswa utawala wake wa juu-chini ya gridi za inje za mitaa na rasilimali za mafuta. Kipaumbele cha nishati pia kinaongozwa na maslahi mapana ya kisiasa. Turkana inaona rasilimali yake ya petroli kama njia kuu ya kutoa changamoto kwa serikali ya kitaifa na kuondoa upendeleo wa kihistoria, na kwa hivyo kuwa na idara ya nishati yenye uwezo ni muhimu kwa malengo haya. Walakini, lengo hili limepata mvuto zaidi kupitia mwingiliano mkubwa wa wadau wasio wa kiserikali, kama kanisa na mashirika ya kijamii ambayo yamekuwa muhimu katika kuhamasisha jamii na kuimarisha upeo wa sauti yao. Hii imesaidia kutoa shinikizo kubwa la chini-hadi juu, kusaidia maendeleo ya uhusiano wa nguvu sawa kati ya kaunti na serikali ya kitaifa kuliko katika zile kaunti zingine tatu.
Pia kuna ishara za utawala wa washikadau wengi huko Nakuru. Kaunti hiyo imepokea msaada wa kujijengea uwezo kutoka kwa watendaji kadhaa wa kitaifa na wa kimataifa wasio wa serikali na kuanza kushirikiana na sekta ya kibinafsi na zile zisizo za kiserekali juu ya maswala ya nishati. Ushirikiano huu unaweza kusaidia maendeleo ya umeme wa gridi ya inje na mipango ya upishi safi ingawa idara ya nishati ya kaunti ina ufadhili mdogo na wafanyikazi duni, ikidhoofisha uwezekano wa hatua hizo. Ugatuzi wa tawala wa nishati haukufaulu sana Migori na Nairobi, ambako idara zake za nishati pia hazina rasilimali nyingi. Katika kaunti ya Migori suala hili linazidishwa na ukosefu wa utaalam wa nishati katika utendaji wa kaunti na uratibu mbaya kati ya idara ya utendaji na idara ya nishati. Huko Nairobi, kupatikana kwa umeme wa gridi ya taifa (licha ya gharama kubwa na kutoaminika) na ukaribu wa serikali ya kitaifa inaonekana kuwa imesababisha nishati kutopewa kipaumbele na utawala wa kaunti, ikifanya ndani ya mji mkuu kuwe na safu ya ziada ya urasimu bila matokeo yanayoonekana wazi wazi51.
Hitimisho
Kwa ujumla, matokeo yanaonyesha kuwa mipango ya utawala ambayo inaunganisha njia zote za ugatuzi na zile za kati imefanya kazi vizuri wakati kikundi kimoja muhimu cha wadau hakijafanya kazi katika nafasi kubwa ya nguvu ikilinganishwa na vingine. Nchini Kenya, hali hii inaonekana wazi katika mwiingiliano wa kaunti na mashirika madogo madogo yasiyo ya kiserikali, na mwiingiliano wa jamii na wadau juu ya haki za ardhi. Walakini, uhusiano huu haujatekelezeka kwa sababu ya udhibiti wa serikali ya kitaifa ambao uimesababisha ukosefu mkubwa wa usawa wa nguvu, ingawa kuna tofauti dhahiri kati ya kaunti.
Serikali ya kitaifa imetumia udhibiti huu kupindukia (na mara nyingi bila upendeleo) kutanguliza masilahi yake ya umeme wa gridi ambayo hufanya kazi kwa sehemu fulani ya watu tu. Kwa hivyo, hitimisho kuu ni kwamba jukumu muhimu la utawala wa nishati uliogatuliwa nchini Kenya ni kukuza na kudumisha mitandao thabiti ya watendaji wa ndani kutoa mizani na ukaguzi mzuri kwa utawala wa "juu-chini", wakati pia ukitetea na kuwezesha suluhisho ya upatikanaji wa nishati inayofaa zaidi vijijini (haswa upishi safi na mipango midogo midogo ya inje ya gridi): bila hiyo, kukosekana kwa usawa wa upatikanaji wa nishati kunaweza kuendelea.
MAPENDEKEZO YA SERA MUHIMU
Kufungua uwezekano wa utawala wa nishati uliogatuliwa kukuza na kudumisha mitandao ya wahusika wa vivijini - jukumu muhimu linalotetewa na jarida hili - yafuatayo yanapendekezwa:
Sheria na kanuni za nishati zilizowazi zikiainisha mahali majukumu yaliyogatuliwa yanaanzia na kuishia, ni muhimu kwa uamuzi-huru katika ngazi ndogo ya kitaifa. Sheria ni bora zaidi kama: ilikuweko kabla ya mamlaka ndogo za kitaifa kuchukua majukumu; ni matokeo ya ushirika wa wadau mbalimbali ambao unawezesha uungwaji mkono na uelewa; na inataja kwa wazi majukumu ya viwango vya chini ili kuepusha usimamizi wa udhibiti mkubwa wa serikali kuu52.
Ujenzi wa uwezo uliogawanywa sawasawa ni muhimu kwa kukuza taasisi za utawala wa nishati uliogatuliwa(na za kati). Hivyo basi vyombo vya sera na uingiliaji zaidi wa wafadhili unahitajika kushughulikia mambo ya uchumi wa kisiasa ambayo yamesababisha kutokua na usawa juu ya wapi na kwa nani msaada huu hutolewa. Msaada unahitaji kufuatiliwa na miongozo wazi ya sheria na uhamishaji wa nguvu ili kuwahamasisha wapokeaji wa kujenga uwezo.
Kuongezeka kwa uhamasishaji wa jamii na watendaji wa serikali na wasio wa serikali juu ya maswala ya nishati na jukumu la jamii katika utawala wa nishati uliogatuliwa ni muhimu sana katika kukuza sera za nishati zinazofaa vijijini na kufanya ukaguzi na mizani kwa sera za serekali ndogo kitaifa na za kitaifa zisizofaa. Bila shinikizo la ngazi ya chini kwenda juu, uwezekano wa utawala bora na uwakilishi wa nishati utapungua sana.
Serikali ya Kaunti kama mwezeshaji badala ya mtekelezaji wa mipango ya nishati. Kufanya kazi kwa kiwango cha karibu zaidi na mitaa, tawala ndogo za kitaifa zimewekwa ili kukuza, kuratibu, na kudumisha mitandao ya wadau wa mitaa kufanya shughuli zinazoongeza ufikiaji wa suluhisho zinazofaa ya nishati vijijini. Hii ni muhimu sana kwani mitandao kama hiyo imekuwa madereva wa msingi wa mipango ya kukuza umeme mdogo wa inje ya gridi na upishi safi - hatua zinazohitajika haraka kushughulikia ukosefu wa usawa wa nishati nchini Kenya na Kusini mwa Jangwa la Sahara.
MAREJELEO
Sieff, R. (2020). ‘Decentralised Energy Governance in the Global South: The Case of Kenya since the Implementation of Devolution’. PhD Thesis. Loughborough University, Loughborough.
2 United Cities and Local Governments (2007). Decentralization and Local Democracy in the World: First Global Report 2007.
3 Bennett, R.J. (1990). Decentralization, local governments and markets: towards a post- welfare agenda. Oxford: Clarendon Press; Donahue J.D. (1997). Disunited States. New York: HarperCollins Publishers Inc.
4 Rodríguez-Pose, A. & Gill, N. (2003). The global trend towards devolution and its implications. Environment and Planning C: Government and Policy. 21(3). pp.333–351.
5 In line with contemporary revisions of Brandt’s (1980) original definition, ‘Global South’ is used to refer to Africa, Latin America, Asia (except Japan, Russian Asia, Singapore, Hong Kong, South Korea and Taiwan), and Oceania (except Australia and New Zealand).
6 Cheeseman, N., Lynch, G. & Willis, J. (2016, p.3). Decentralisation in Kenya: the governance of governors. Journal of Modern African Studies. 54(1). pp.1-35.
7 IEA (2020). SDG7: Data and Projections
Access to Electricity. International Energy Agency, Paris.
8 World Health Organisation (2018). Household air pollution and health. [Online]. Available from: https://www.who.int/en/news-room/fact-sheets/detail/household-air-pollut.... [Accessed: 24 January 2019].
9Africa Progress Panel (2015, p.23). Africa Progress Report 2015.
10Bigsten, A. & Moene, K.O. (1996). Growth and Rent Dissipation: the Case of Kenya. Journal of African Economies. 5(2). pp.177–98; Africa Progress Panel (2015). Africa Progress Report 2015.
11 Scott, A. (2015). Building electricity supplies in Africa for growth and universal access. Background paper for Power, People, Planet: Seizing Africa’s energy and climate opportunities. New Climate Economy, London and Washington, D.C.
12 IEA (2019) Africa Energy Outlook 2019. International Energy Agency, Paris.
13 13. Batchelor, S., Brown, E., Scott, N. and Leary, J. (2019). Two birds, one stone—reframing cooking energy policies in Africa and Asia. Energies, 12(9), p.1591.
14 Batchelor, S. and Smith, J. (2014). Beyond Literacy and Knowledge: Energy Proficiency for Decentralised Governance. Working Paper 3, Project EP/L002469/1; Brown, E., Cloke, J. & Harrison, J. (2015). Governance, Decentralisation and Energy: a Critical Review of the Key Issues. Working Paper 1, Project EP/L002469/1; Havet, I., Chowdhury, S., Takada, M. & Cantano, A. (2009). Energy in National Decentralization Policies. United Nations Development Program (UNDP).
15 Brown, E., Cloke, J. & Harrison, J. (2015, p.4). Governance, Decentralisation and Energy: a Critical Review of the Key Issues. Working Paper 1, Project EP/L002469/1.
16 Brown, E., Cloke, J. & Harrison, J. (2015). Governance, Decentralisation and Energy: a Critical Review of the Key Issues. Working Paper 1, Project EP/L002469/1, April 2015.
17 Goldthau, A. (2014). Rethinking the governance of energy infrastructure: Scale, decentralization and polycentrism. Energy Research and Social Science. 1. pp.134–140.
18 Goldthau, A. (2014, p.134). Rethinking the governance of energy infrastructure: Scale, decentralization and polycentrism. Energy Research and Social Science. 1. pp.134–140; Sovacool, B.K. (2011). An international comparison of four polycentric approaches to climate and energy governance. Energy Policy. 39(6). pp.3832–3844.
19 World Bank (2015, p.1). Kenya’s Devolution [Online]. Available from: http://www.worldbank.org/en/country/kenya/brief/kenyas-devolution. [Accessed: 7 December 2017].
20 Kangu, J.M. (2015). Constitutional Law of Kenya on Devolution. Nairobi: Strathmore University Press.
21 Cheeseman, N., Lynch, G. & Willis, J. (2016, p.3). Decentralisation in Kenya: the governance of governors. Journal of Modern African Studies. 54(1). pp.1-35.
22 ‘Grid islands’ is used here to refer to (usually larger) off-grid electricity systems which are structurally ‘off-grid’ (as they are not connected to the main grid), but are ‘grid’ from a governance perspective as they are subject to the same centralised KPLC control – e.g. on matters such as tariffs and service. See Sieff, R. (2020).
23 IEA (2019). Africa Energy Outlook 2019. International Energy Agency, Paris.
24 Lee, K., Brewer, E., Christiano, C., Meyo, F., Miguel, E., Podolsky, M., Rosa, J. and Wolfram, C. (2016). Electrification for “Under Grid” households in Rural Kenya. Development Engineering. 1, pp.26-35.
25 The East African Centre of Excellence for Renewable Energy and Energy Efficiency (2019). EACREEE Consultation Meeting on Energy Efficiency with Ministry Representatives. Dar es Salaam; Kamau, M. (2019). Why your power bills remain high despite cheaper generation. The Standard Digital. [Online]. 14 May. Available from: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001325363/transmission-losses-a.... [Accessed 12 June 2019].
26 Alupo, G.A. (2018). Kenya National Electrification Strategy: Key Highlights 2018. World Bank.
27 Clean Cooking Alliance (2020). Kenya. [Online]. Available from: https://www.cleancookingalliance.org/country-profiles/focus-countries/4-... [Accessed: 10 May 2021]
28 IEA (2019). Africa Energy Outlook 2019. International Energy Agency, Paris.
29 Kangu, J.M. (2015). Constitutional Law of Kenya on Devolution. Nairobi: Strathmore University Press.
30 Interviews conducted with representatives from REREC, KPLC and the Council of Governors in 2017.
31 Government of Kenya. The Energy Bill, 2015. (2015).
32 Interviews conducted with senior energy consultants from the Stockholm Environment Institute and a Kenyan energy consultancy in 2017.
33 Parastatals refers to semi-autonomous public entities. There are nine energy parastatals in Kenya: Kenya Power and Lighting Company (KPLC), Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA), Geothermal Development Company (GDC), Kenya Electricity Generating Company (KenGen), Kenya Electricity Transmission Company (KETRACO), Rural Electrification and Renewable Energy Corporation (REREC), Kenya Nuclear Electricity Board (KNEB), Kenya Pipeline Company (KPC), Kenya Petroleum Refineries Limited (KPRL)
34 The ‘oversight’ covers all off grid systems except those which are for own use (e.g. solar home systems). See Day, T., Kurdziel, M.-J. & Barasa, M. (2018). The role of renewable energy mini-grids in Kenya’s electricity sector. New Climate Institute.
35 Ockwell, D. and Byrne, R. (2017). Sustainable Energy for All: Innovation, technology and pro-poor green transformations. Abingdon, Routledge.
36 Byrne, R., Onsongo, E., Onjala, B., Chengo, V., Todd, J.F., Ockwell, D. and Atela, J. (2020). Electric cooking in Kenya: an actor-network map and analysis of a nascent socio-technical innovation system [Online]. Available from: https://mecs.org.uk/publications/electric-cooking-in-kenya-an-actor-netw... [Accessed: 9th October 2020]
37 A case in point of stringent oversight and failure to align energy legislation with the Constitution is Remba island (Homa Bay), a location not grid-connected, where ERC disconnected a private sector mini-grid supplying 10,000 residents, stating the system lacked the permit required by the Energy Act 2006. ERC (2018). Twitter. [Online] Available from: https://twitter.com/EPRA_Ke/status/974351029889388544
38 The largest national government led initiative in grid electricty, the US$783M Last Mile Connectivity Project, is dwarfs that for off-grid electricty, the US$150M Kenya Off-Grid Solar Access Project (KOSAP) and for clean cooking, the US$31M Mwananchi Gas Project. World Bank (2019). Projects. [Online]. 2019. Available from: http://projects.worldbank.org/search?lang=en&searchTerm=kenya. [Accessed: 29 April 2019]. Anyanzwa, J. (2018). Kenya’s cooking gas project for the poor burnt up by graft. The East African. [Online]. 21 October. Available from: https://www.theeastafrican.co.ke/news/ea/Kenya-cooking-gas-project-for-t.... [Accessed: 29 April 2019].
39 Wafula, P. (2017). Plan to split Kenya’s energy docket generates heat among top ministry officials. The Standard. [Online]. 2 November. Available from: https://www.standardmedia.co.ke/business/article/2001259099/state-mulls-.... [Accessed: 17 April 2018].
40 Musau, N. (2018). How two cabinet secretaries control electric poles tenders. The Standard. [Online]. 28 July. Available from: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001289731/revealed-the-two-cabi.... [Accessed: 1 May 2019].
4 Sieff, R. (2020).
42 Feedback from 38 counties at the National Energy Trust Fund (NETFund) county renewable energy workshop in Naivasha in December 2017.
43 Interview conducted with senior officer from GIZ in 2017
44 Interview conducted with CAFOD representative in 2019.
45 Conversations with representatives from
United Nations Environment Programme, United Nations Industrial Development Organisation and the Technical University of Denmark (DTU) in 2017.
46 Interviews conducted with representatives from the World Wide Fund for Nature and CAFOD in 2017.
47 Examples of such projects include the Lake Turkana-Suswa transmission line, the Kinangop Wind Power project, and the Meru Wind Power Station.
48 Olonyi, L. (2019). Kenya could do without coal’s poisonous legacy. Business Daily. [Online]. 21 April. Available from: https://www.businessdailyafrica.com/analysis/ideas/Kenya-could-do-withou.... [Accessed: 3 May 2019].
49 Focus groups conducted in six communities across three counties (Migori, Nakuru, and Turkana) in 2017.
50 Focus groups conducted in six communities across three counties (Migori, Nakuru, and Turkana) in 2017. Interviews with representatives from KETRACO and Migori County Government in 2017. See also Johnson, O., Nyambane, A., Cyoy, E. & Oito, L.G. (2016). County Energy Planning in Kenya: Local Participation and Local Solutions in Migori County. Stockholm Environment Institute.
5 Research and analysis in this section: Sieff, R. (2020).
52 Ribot, J.C. (2002). Democratic Decentralization of Natural Resources: Institutionalizing Popular Participation. Washington DC: World Resources Institute; Buckland, H. Eales, A. Brown, E. Cloke, J. Blanchard, R. Yona, L. Zalengera, C. Batchelor, S. Sieff, R. Nyirenda, E., Bayani, E. (2017). Malawi District Energy Officer Blueprint: Recommendations Paper. The University of Strathclyde, Glasgow.
Maelezo ya Mawasiliano
Dk. Richard Sieff
Mshirika wa Utafiti
Jiografia na Mazingira ; Chuo ki Kuu cha Loughborough, Njia ya Epinal, Loughborough LE11 3TU Uingereza.
Barua pepe: R.Sieff@lboro.ac.uk
Dr. Richard Sieff
Research Associate
Geography and Environment, Loughborough University, Epinal Way, Loughborough LE11 3TU United Kingdom
Email: R.Sieff@lboro.ac.uk